NyumbaLink TZ

Sera ya Faragha

Imesasishwa mwisho: 16 Julai 2026

NyumbaLink TZ ("app", "sisi") ni jukwaa la kutafuta na kutangaza nyumba, viwanja na miradi ya makazi Tanzania, pamoja na zana za usimamizi wa wapangaji kwa wenye nyumba na mawakala. Sera hii inaeleza data tunayokusanya, tunavyoitumia, na haki zako.

1. Data tunayokusanya

  • Taarifa za akaunti: jina, barua pepe, namba ya simu (hiari), picha ya wasifu, lugha unayopendelea.
  • Maudhui unayoweka: matangazo ya nyumba/viwanja (picha, video, maelezo, bei na eneo/koodineti za tangazo), posts, reviews, comments na ujumbe wa chat.
  • Kumbukumbu za usimamizi: wenye nyumba/mawakala wanaweza kuweka kumbukumbu za wapangaji, mikataba, malipo ya kodi na matengenezo. Kumbukumbu hizi zinaonekana kwa mwenye nyumba aliyeziweka na (panapohusika) mpangaji aliyeunganishwa.
  • Uthibitisho (KYC): watangazaji wanaoomba beji ya uthibitisho wanaweza kuwasilisha namba ya NIDA au leseni ya biashara. Hukaguliwa na admin pekee.
  • Data ya kiufundi: token ya arifa (push notifications), ripoti za hitilafu (crash reports), na taarifa za msingi za kifaa kwa ajili ya kuboresha huduma.

App haipokei wala kusafirisha pesa — kumbukumbu za malipo ni maandishi ya kumbukumbu tu yanayowekwa na kuthibitishwa na mwenye nyumba. Hatukusanyi taarifa za kadi au akaunti za benki.

2. Tunavyotumia data

Hatuuzi data yako kwa mtu yeyote.

3. Watoa huduma tunaowatumia

  • Google Firebase — akaunti (Authentication), hifadhidata (Cloud Firestore), na huduma za seva. Data huhifadhiwa kwenye seva za Google.
  • Cloudinary — kuhifadhi picha, video na nyaraka zinazopakiwa.
  • Resend — kutuma barua pepe za mfumo (mf. uthibitisho wa akaunti) kutoka no-reply@nyumbalinktz.com.
  • Expo — kutuma arifa (push notifications).
  • OpenStreetMap / Nominatim — ramani na kutafsiri koodineti kuwa anwani (geocoding). Koodineti za eneo la tangazo hutumwa kwa huduma hii.
  • Google Sign-In — ukichagua kuingia kwa Google, tunapokea jina, barua pepe na picha ya wasifu kutoka Google.

Watoa huduma hawa wanachakata data kwa niaba yetu tu, kwa mujibu wa mikataba na sera zao za faragha.

4. Data inayoonekana kwa wengine

5. Usalama

Data yote husafirishwa kwa muunganiko uliosimbwa (HTTPS/TLS). Upatikanaji wa hifadhidata unadhibitiwa na sheria za usalama (security rules) zinazobana kila mtumiaji kwenye data yake. Nywila zako zinahifadhiwa na Firebase Authentication — hatuzioni wala kuzihifadhi sisi.

6. Kufuta akaunti na data

Unaweza kufuta akaunti yako moja kwa moja ndani ya app: Mipangilio (Settings) → Akaunti → Futa Akaunti. Hii inafuta akaunti yako ya kuingia na data zako (wasifu, matangazo, kumbukumbu, chats) mara moja. Maelezo kamili: nyumbalinktz.com/delete-account.

Tunaweza kubakiza kumbukumbu chache kwa muda mfupi pale inapohitajika kisheria au kuzuia udanganyifu.

7. Watoto

Huduma hii haielekezwi kwa watu chini ya miaka 18.

8. Mabadiliko ya sera

Tukibadilisha sera hii, tutasasisha tarehe iliyo juu na, kwa mabadiliko makubwa, kutoa taarifa ndani ya app.

9. Wasiliana nasi

Maswali ya faragha au maombi ya data: weisikosilvester@gmail.com